Mamilioni ya waombolezaji walikusanyika katika Msikiti wa Jamkaran mjini Qom kushiriki katika marasimu ya kumuaga na kumuenzi Shahidi Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, huku Sala ya Maiti ikiongozwa na Ayatollah Javadi Amoli.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Mamilioni ya waombolezaji wamejitokeza katika mji mtakatifu wa Qom kushiriki katika marasimu ya kumuaga na kumuenzi Shahidi Ayatollah Sayyid Ali Khamenei.
Marasimu hayo yamefanyika katika Msikiti maarufu wa Jamkaran, ambapo umati mkubwa wa waumini ulifurika eneo hilo kutoa heshima zao za mwisho. Sala ya Maiti imeongozwa na Ayatollah Javadi Amoli, huku waombolezaji wakisali na kumuombea marehemu kwa unyenyekevu na majonzi makubwa.
Mahudhurio hayo makubwa yameonyesha mapenzi, heshima na mshikamano wa wananchi pamoja na waumini waliojitokeza kushiriki katika hafla hiyo ya kihistoria.

Your Comment